Jumatano, 26 Oktoba 2016

Mkamilo: Manji tuachie Yanga Sc, anzisha yanga yako

Usemi huu ni hakika na kweli, na sasa unatimia hapa Yanga Sc. mhh " akili ni zaidi ya mali" msemo huu!!!!!
hapa huna haja ya kuuliza kwa nini akili ni zaidi ya mali kwa hiki kinachoendelea katika clabu yetu ya Yanga timu inayopendwa na kujulikana na kila rika, hata mtoto wa miaka mitatu atakwambia napenda Yanga, sasa katika hili nami sitanyamaza kutoa yaliyo moyoni kuwa, mr. Manji kwa mtindo huo achana nasi.
Jamani hata hili jambo kuna haja na kukaa na wasomi kujadili? kuna haja ya kufumbafumba maneno?  kwani Mr. Manji nawe umeanza siasa? lakini katika hayo yote najiridhisha kuwa huenda eilimu ya mpira umeisahaun lakini pia siamini kama wewe Manji kwa sababu zinazosikika kuwa unaweza kufanya haya yote, isipokuwa kama ni kweli hebu rudi nyuma na tafakari kwa makini sana ikiwezekana jipatie likizo ya wiki 2 upumzike na kutuliza akili ili kwa utulivu huo upate lililo zaidi ya ulilofikiri hapo awali, lakini kwa nini nimlaumu Manji pekee? kwani Yanga hakuna viongozi? katibu na mwenyekiti msaidizi ni kweli mmekaa na kukubaliana hayo? mnaweza kutuambia ni sababu gani ya msingi sana ya kufanya hayo mliyoamua? kabla la kwanza halijaisha ninyi mnaibuka na jambo jingine gumu tena lenye athali kubwa kwa timu . hivi hamuoni kuwa mnazidi kuleta matatizo? mpo hapo kwa ajili ya kusema "ndio mzee"  sasa ndipo usemi unapokamilika kuwa ni " akili ni zaidi ya mali"hata anayeijua Yanga leo hii ukimsimulia sinema hii atakwambia sinunui ng'o!! kwa kweli viongozi Yanga hamjatendea haki nafasi zenu tu kama jambo hili ni la " ndio mzee"  sasa mimi nisiyekuwa msomi wa mpira naomba ninyi wasomi mniambie ni sababu gani ya msingi iliyowafanya msitishe mkataba wa mzee Hans Van Der Pluijm? hakuna anayeweza kuamini kuwa katika mechi tisa alizoanza nazo kwa mkataba wake mpya wa miaka miwili kudroo mechi tatu na kufungwa moja ndizo zimewafanya muone kuwa hana ubora, ni nini hapo? mbona hamjamfukuza Chirwa mliyemsajilii kwa milioni 200 na kufunga magoli mane hadi sasa? hamuoni Mun united japo wamemsajili Pogba kwa paund milioni 100 na hadi sasa kafunga magoli manne tu mmesikia wanamtema? mpira wenu ni wa wapi wabongo? amewakosea nini mzee Hans Van Der Pluijm?  tafadhali acheni siasa katika soka, eti mara tunataka kocha wa kufundisha fizikia katika michezo, hivi kwa  kocha kama Pluijm mnadhani ni wa kubabaisha kama zilivyo siasa za Bongo ambazo Mh. Magufuli ameamua kuja kuzifutilia mbali? ngoja aje na huko, msione yuko kimya anawatega tuu, na hivyo ni chama lake utafika muda wake,
        Viongozi Yanga acheni kuiga mambo, kocha Pluijm ana mikakati yake, mbona msimu uliopita hamkusema mnataka afundishe fizikia wa wachezaji? au leo nani kaenda kusoma na kuja hapo na jipya hilo? mwacheni yeye ana ratiba katika kazi yake. kwani katika katika mkataba si ni kuna masharti ya mkataba ikiwemo kutetea taji la ubingwa ligi kuu? sasa mechi kumi zimemaliza ligi hiyo? duuu!!! kweli "akili ni zaidi ya mali" kama mlivyovunja benchi la ufundi na ninyi viongozi wte ukianza mjiuzulu. kila mtanzania anafahamu mchango wa Puijm katika soka la tanzania hata serikali inajua hilo sasa ninyi ni akina nani tena kwa mechi kumi? msimu uliopita amekuwa kocha bora Tanzania na kuwavutia  kuna habari zinasiika eti kwa kuwa alimkataa Mrisho ngassa sasa bossi Manji akachukia na kutaka kulipa kisasi. hivi unawezaje kumfananisha Mrisho  Ngassa na Pluijm? jamni kuna haja ya kwenda darasani kwa ajili ya kujibu hili? nawaomba mrudisheni mzee atetee ubingwa huyo Lwandamina wenu asajiliwe na Taifa Stars, hakuna haja ya kumleta jangwani.
                                  Naipenda Yanga lakini sitaki kuumwa

Jumatatu, 17 Oktoba 2016

Herman "Sadaka yako ndiyo hukumu yako"

Na ahimidiwe MUNGU zaidi kushukuriwa kwa yote mazuri atutendeayo sisi wadhambi katika mwili na roho,
Namshukuru mwana wa MUNGU Bwana kmkombozi  wangu kwa kuendelea kujitoa sadaka kuu kwa ajili ya kuiokoa roho na maisha yangu,
Nawashukuru wazazi kwa kunileta duniani na kunilea katika maadili mema yanayompendeza MUNGU na wanadamu wote,
Nawashukuru ndugu jamaa na marafiki na watu woote kwa kuwa ninyi mmenikomaza kutoka ubichi.
              kwa kadiri ya mapenzia ya MUNGU, akujalie unayebahatika kufungua ukurasa huu na kupata angalau ujumbe ninaotamani kwa hamu kubwa ukufikie ili kama ulikosea katika hili urekebishe.
     ninatamani kwa kuwa ninawapenda sana na ninamshukuru MUNGU zaidi kwa kuwa amenijalia kumpenda kila mtu kwa kadiri ya mapenzi yake.
        SADAKA. mara nyingi wengi tumefikiri kuwa sadaka ni ile pesa tunayoitoa kila siku ya ibada kwa kila dini na madhehebu, lakini kwa MUNGU hakuna tofauti ya maana kwa sadaka kwa dini na madhehebu yote, natamani nishirikishe kidogo namna ya utoaji wa sadaka, ni ipi namna nzuri ya kutoa sadaka kwani sadaka ni jambo muhimu sana katika ustawi wa maisha yetu ya kiroho, umuhimu wa jambo hili unatokana na hata asili ya uumbaji na kanuni za MUNGU mwenyewe. tangu asili MUNGU amependa kila mtu amtolee sadaka safi yenye kumpendeza itokayo moyoni na si mfukoni kwani iko tofauti kubwa kati ya hizi sadaka mbili ile ya mfukoni na ya moyoni.sadaka safi impendezayo MUNGU ni lazima iguse moyo wako tena kwa maandalizi si kuito mfukoni na kuiweka mahala pa kutolea, hapo ni sawa na kuchukua mahindi na kuyaweka gharani, na huo ndio ukweli, sadaka lazima isemewe kitu kutoka moyoni ili kupitia hiyo imguse MUNGU na kukuongeza zaidi.
           Sadaka si kitu cha kukitoa kama unatoa pesa kununua karanga sokoni, bali sadaka  ina thamani kubwa kwa MUNGU hivyo ni vyema unapoitoa uiandae kwanza ndipo ukamtolee kwa unyenyekevu wa moyo,MUNGU anapenda sana sadaka si kwamba ni masikini kuwa hana hela, kwanza sadaka si laziam iwe hela au mahindi, mchele n.k. .
Tazama umuhimu wa sadaka na thamani ya sadaka, MUNGU anaitazama sadaka kuwa ni kitu cha pekee sana, anaona hakuna kiu kitakachoweza kumwokoa mwanadamu kutoka katika utumwa ila ni damu, tena si damu tu, ila ni damu ya mwanadamu aliyemfanya yeye mwenyewe, unajua kuwa hiyo ni sadaka?? anamtuma YESU KRISTO  afe ili kupitia kifo hicho mwanadamu mdhambi aokolewe, si hapo tu, MUNGU anamtuma Abrahamu amtoe mtoto wake wa uzeeni awe sadaka ya kuteketeza, ni jinsi gani anaithamini sadaka na kuiona kuwa ni kitu cha pekee sana??
           Tazama MUNGU mwenyewe anaseama "nijaribuni kwa sadaka/matoleo muone kama sitawafungulia milango ya mbinguni"(malaki 3:11)  kwa sadaka na matoleo safi anatuhakikishia kuwa atatufungulia milango ya mbinguni ila unatoaje mpendwa?? ni kweli kuwa wengi tunajitahidi sana kutoa sadaka na matoleo  isipokuwa tunatoa bila kuyapa umuhimu, tunayatoa ili kutimiza wajibu na kanuni tu ya makanisa na miskiti yetu, lengo la sadaka si kutimiza haya ila ni kuamini kuwa MUNGU anapenda tumtolee kama anavyotujalia.
         unapotoa sadaka yako kabla hujaitoa hebu sema kitu kwa ajili ya sadaka yako ukianza kwa kumshukuru  KUNGU kwa yote aliyokutendea kwa kipindi fulani na kwa mambo fulani, sadaka ni lazima uiombee tena uiandae maalumu na sio kukurupuka na kuitoa kama unanunua samaki. pia toa sadaka kwa moyo wa furaha na mapendo, toa sadaka yako inayogusa moyo wako tena kwa hiari yako, usitoe sadaka kama ziada ya mahitaji yako, katika mambo yako sadaka iwe jambo la kwanza ndipo na mengine yafuate, usitoe sadaka ya kile kilichozidi au faida. YESU anawaambia kusanyiko kuwa "mama huyu mjane ametiazaidi katika hazina yake kuliko watu wotekwa maana wenguine wametoa sadaka zao kutokana na ziada ya mali zao: (luka 21:2, marko12:41-44) japokuwa mjane yule alitoa kidogo lakini kiligusa moyo wake na YESU pia kwani alitoa kwa moyo kile kilichokuwa tegemezi kwake ila wengine walitoa zilizokuwa faida.
        unapotoa sadaka yako hakikisha huna tatizo na mtu ili MUNGU aipokee na kuibariki tele, hakikisha una amani na kila mmoja, sio umegombana na mtu unakwenda kutoa sadaka, hiyo si sadaka safi kwa MUNGU imeandikwa "Kwanza ukapatane na ndugu yako ndpo urudi unitolee sadaka yako"(mathayo 5;23-24)
             ndugu yabngu kwa kuwa sadaka ni jambo muhimu sana kwetu tutoe kadiri MUNGU anavyotujalia
              karibu tena kwa kujadili juu ya sadaka na utoaji
wako Herman mkamilo,
MUNGU akubariki sana

Jumamosi, 15 Oktoba 2016

MENEJA:"Lazima turudi na ndoo leo"

 Hivi ndivyo unavyoweza kuona jinsi gani kikosi cha  KSC kilivyokuwa kikijiamini kwa mchezo wa fainali ya ligi wilaya Muleba uliomalizika dakika chache zilizopita, bila shaka utakumbuka safari ya KSC iliyojawa na mitihani likuki lakini hapo unapowaona ni kama wamemaliza kazi waliyokusudia, kila mtu ana furaha, kulikuwa na kazi kubwa sana. si rahisi kumwona mtu mwenye cheo  cha Umeneja kuvaa kama mchezaji na kujichanganya na wachezaji huku akifanya baadhi ya vituko, lakini hayo yote ni kwa sababu ya furaha aliyokuwa nayo leo. achilia mbali makoach wote wamekuwa na shangwe sana japo wanakwenda kumalizia fainali kitu ambacho Meneja amesema "Lazima turudi na ndoo" sasa sijui aliiweka wapi!!!


Furaha ilizidi sana hata wengine kusahau kuwa kuna kazi mbele yao, kuna wakati beki mmoja kijana Davis alianza kucheza muziki kama yuko ukumbini kumbe anasubiri mchezo, kocha aliamua kumuacha kila mtu afurahi bila mipaka akiamini kuwa wamestahili kwa kazi waliyoifanya.hapakuwa na tatizo lolote kiafya na kila mchezaj alisema yuko kamili kwa kila kitu kwani ni lazima washinde,
          baadhi ya wachezaji walionekana kuwa kimya sana kana kamba kuna mambo wanafikiria. walijiandaa na kwenda kula katika hoteli yao tayari kwa safari, walisafiri salama  na kufika salama, maandalizi ya mchezo yalianza na mchezo kuanza baada ya mkuu wa wilaya kufungua rasmi,
            mchezo ulianza kwa kasi sana kila timu ikijilinda imara lakini dakika ya 23 Vatican walipata goli l la kuongoza kupitia piga nikupige ya mpira wa kona hadi ukaingia wavuni, lakini dakika ya 40 KSC ilisawazisha kupitia penalt iliyopigwa na kapilima. hadi mapumziko magoli yalikuwa vatican 1 1 KSC kipindi cha pili kilianza kwa kasi vilevile na dakika ya  ya 74 Vatican walipata goli la pili kwa penalt baada ya mchezaji wao kufanyiwa madhambi katika eneo la kipa, na hadi mchezo unamalizika Vatican ndio walikuwa washindi na mabingwa wa wilaya kwa mwaka 2016
          baada ya mchezo kuisha mkuu wa wilaya aligawa zawadi za ushind na kisha KSC kuondoka, kpumzika wiki 2 ili waanze kujiandaa kwa lig ya mkoa inayotarajiwa kuanza 12 Dec 2016.

                                                                                    kaa hapohapo Mkamilo89.blogspot.com

Jackson M:Wamepitia tundu la sindano

Amini usiamini hali ya uwanja wa Zimbihile katika mchezo fainali iliyowakutanisha Vatican FC na Kamachumu SC ilikuwa si ya kawaida kana kwamba watu walikuwa wakiitazama mechi ya watani wa jadi(simba na yanga) uwanja ulijaa mapeam san atofauti na ilivyokuwa katika mchezo wa nusu fainal. watu walikuja kwa uchu mkuu kuona ni nani atibuka bingwa wa wilaya kwani kila timu ilijigamba kuwa inaweza kumtandika mwenzake, tumezoea kuwa timu wenyeji ndio inakuwa na mashabiki wengi zaidi lakini kwa jana wageni ndio walikuwa na mashabiki 75% walipofunga  KSC uliona jinsi uwanja ukishangilia kwa nguvu sana, 
        Hali ya mchezo haikuwa mbaya kwani hakuna aliyeumizwa, na waamuzi walichezesha vixuri, mwisho wa mchezo mkuu wa wilaya ya Muleba alianza kugawa zawadi ya ushindi kwa washindi, baada ya kuamliza zoezi hilo timu ya KSC ilijandaa kurudi mjini kwao Kamachumu lakini kocha msaidizi alisikika akisema "Wamepitia tundu la sindano" na kuongeza kuwa "tunakwenda kujipanga ligi ya mkoa ambayo kwa kocha mkuu ilikuwa plan yake namba moja, amefanikisha hilo sasa anakwenda kuonesha taaluma yake mkoani, hali itakuwaje? kuna nini atafanya tumsubiri kwani amewapa wachezaji mapumziko ya wiki 2 kisha kurudi kuanza upya mazoezi tar 31October 2016 kwa ajili ya ligi y mkoa inayotarajiwa kuanza 12/12/2016 katika uwabja wa Kaitaba mjini Bukoba, nami,
        Nami nawatakia mapumziko mema, msisahau mazoezi mepesi kwa ajili ya afya zenu.
                                                                      Mkamilo89.blogspot.com

Jumatatu, 10 Oktoba 2016

KOCHA SIDO: Walichonifanyia KSC Sitawasahau maishani

Kwa kushindwa kujizuia, kocha mkuu wa timu ya SIDO iliyopo mjini Muleba leo ndio mara yake ya kwanza kuumizwa kwa timu yake tangu ameanza kuifundisha, leo  tar 10 October 2016 ulichezwa mchezo wa nusu fainali kati ya timu ya KSC  ya Kamachumu na SIDO ya mjini Muleba katika dimba la Zimbihile, ni mchezo uliokuwa ukisubiliwa kwa hamu sana na mashabiki wengi kutoka maeneo mbalimbali ya mji wa Muleba, mwamuzi alianzisha pambano hilo ambapo mpira ulianza kwa utulivu kwani kila timu ilionekana ikiiogopa nyingine.Iliwachukua dakika 22 timu ya KSC kubadili hali ya hewa ya dimba la Zimbihile pale ambapo kijana mdogo Mlekwa kuutumbukiza mpira golini akipokea pasi nzuri ya 'non-stop engine' Ramso na mashabiki wengi wa KSC kusimama ya kushangilia huku wakiamini kuwa kazi imekwisha, SIDO walifanya mabadiliko haraka sana ili angalau kurudisha goli kabla ya mapumziko, lakini haikuzaa matunda, hadi dakika 45 za kipindi cha kwanza kinamalizika KSC 1- 0 SIDO
      Makocha wa timu zote walifanya mazungumzo na vikosi vyao na kisha kurejea uwanjani kumalizia dakika 45 za lala salama, mpira ulianza kwa kasi sana huku KSC wakijilinda na SIDO wakishambulia kwa kasi sana wakitaka kusawazisha, mipango yao ilikamilka na kupata goli dakika ya 10 ( dakika ya 55 ya mchezo) ya kipindi cha pili kupitia kona nzuri iliyowaacha mabeki wa KSC wakihadaa na mchezaji wa SIDO kupata nafasi ya kupiga kichwa huru(free header) bila kukabwa na yeyote mpira ukaingia wavuni, sasa hali ya mchezo ikabadilika na vijana wa kocha Masimango wakaanza kujihami ili wasiruhusu goli lingine kwani wapinzani walionekana kuwa makini sana, kocha Masimango alianza kuwapanga vijana wake kwani alishawaona wameanza kupotea mchezoni, baada ya dakika 9 kupita SIDO waliandika goli la pili, kitu ambacho kiliwachanganya KSC lakini kocha wao aliendelea kuwahimiza kwa kuwaambia "hapa hadi dakika 90 kitaeleweka, hali ilizidi kuwa mbaya kwa KSC kwani SIDO waliwafanya kama watumwa wao, kuna vioja kipa wao alivifanya viilimuumiza sana  kocha Masimango baada ya kudaka mpira na kukaa na kuanza kupiga danadana, huku refa asichukue hatua yoyote na muda kuisha , dakika ya 76 kocha msaidizi  wa KSC( Jackson M) alifanya mabadiliko ya haraka kwa kumtoa mtoa pasi  ya goli na kumpa nafasi kijana machachari Daudi kila mtu hakuamini maana ya badiliko lile lakini kocha Jackson ndiye alijua, dakika ya 86 alipewa kadi njano kwa kile alichodai refa kuwa alimdanganya kuwa kapgwa kofi na mchezaji wa SIDO, dakika zilikuwa zikimalizika lakini KSC walifanyakazi waliyoambiwa na kocha wao kuwa hadi filimbi  ya mwisho ndio mpira umekwisha, dakika 90 zilikamilika na dakika 2 kuongezwa , wakati ambao kila mtu aliamini kuwa KSC ndio mwisho wa safari, lakini ni yuleyule kijana daudi kwa utundu alitafakari afanye nini akasema "baba bora nipate red lakini nikiguswa kidogo naanguka nipate penalt"hakiuna aliyejua mawazo ya kijana huyu, dakika ya 81 beki wa SIDO alimzoa Daudi vibaya sana na hapo refa kumpa zawadi ya red akapumzike salama, na mpira wa faulo upigwe kuelekea lango la SIDO, unalikumbuka goli la Kichuya lililoharibu pilau la Yanga 01 October pale Taifa? ni Mashoto J alipiga faulo ile na kuuzamisha mpira moja kwa moja wavuni, unajua nini kilitokea hapo? mpira unawekwa kati na mwamuzi anapuliza kipenga kuashria mpira umekwisha,
      Bila kupoteza muda kwa kuwa nusu fainali iliamriwa kuzipiga dakika 30 nyingine, vijana wa Masimango waliingia wakijiamini sana na kusema kuwa kazi imekwisha, walianza dakika 15 za kwanza kwa kasi kila mtu akitaka kumaliza kazi bila kuingia katika matuta, ziliisha zile 15 za kwanza bila mabadiliko ya yoyote, zilianza nyingine 15 za pili nazo kuisha bila mbabe ndipo muda wa matuta kufikia, sasa hapo hakuna mjanja kwani ni mchezaji na kipa tu.makocha  waliita vikosi vyao na kuwaelekeza mbinu za mwisho kama ujuavyo mwalimu hachoki kufundisha mwanafunzi wake,  walianza penati kama ifuatavyo:

  1. KSC- Kaijage=goooo!!!                   SIDO=gooo!!!
  2. KSC-Kapirima=goooo!!                   SIDO=gooo!!!
  3. KSC-Moses=gooo!!!                        SIDO=gooo!!!
  4. KSC-Florian=gooo!!!                       SIDO=goo!!!!
  5. KSC-Kayana=gooo!!!                      SIDO=amekosaaa!!!
Hapo maneno ya kocha Masimango yalitimia kuwa ni "lazima vijana wangu muende Kaitaba japo si rahisi" hapo mwamuzi aimaliza mchezo na uwanja kufulika watu wote bila kujali kuwa ni wa SIDO au mafunzo au Vatican, kila mtu alishangilia kwani ni ushindi wa ubabe tu, kweli KSC wana haki n kila sababu ya kupongezwa, wamefanya kibarua kigumu sana. daktari wa timu alijaribu kumsalimia kocha mkuu wa SIDO  kwani tangu amefika hakupata nafasi kutokana na ubize aliokuwa nao, mazungumzo yao yalikuwa hivi

  • Daktari KSC- kocha habari za majukumu na pole 
  • Kocha SIDO- Nzuri na Nishapoa!
  • Daktari KSC- umepokeaje matokeo ya leo?
  • Kocha SIDO- ni kawaida tu daktari ila kiukeli nimeumia sana kwa vijana wangu.
  • Daktari KSC- kwanini kocha, mbona vijana wamepambana sana?
  • Kocha SIDO- wamejitahidi si kwamba wamecheza nilivyotaka mimi.
  • Dakatri KSC- je ushindani umeuonaje, unasemaje vatican wakoje?(daktari anachimbua)
  • Kocha SIDO- Mhh!!! daktari siwezi sema katika hilo ila mnaweza shinda mkirekebisha viungo wenu
  • Daktari  KSC- sawa kocha nashukuru niwatakie kazi njema na mtuombee nasi tushinde fainali 
  • Kocha SIDO- usijali, ila jamani walichonifanyia KSC sitasahau maishani.(polepole anaondoka)
kifupi hali ndivyo ilivyokuwa siku ya leo katika dimba la zimbihile
    usikose kutembelea: mkamilo89.blogspot.com
   

Jumapili, 9 Oktoba 2016

Kwa kombinesheni hii, Sido mtautafuta mpira kwa tochi mchana kweupe!!!




Wakati yakiwa yamebaki masaa 22 kuanza kwa mechi za nusu fainali. joto la mechi hizo limepanda moto kwa kiasi kikubwa sana tofauti na miaka yote, lakini cha ajabu kocha msaidizi wa KSC Jackson M  ameviangalia vikosi vyote vilivyoingia nusu fainai na kusena kuwa 'Kaitaba ni lazima', kauli hiyo ameitoa msaidizi huyo ikiwa ni siku chache tangu asikike kocha mkuu Masimango Ph kusema, anafananisha umbali wa safari ya kwenda kaitaba ligi ya mkoa ni kama Kamachumu na mafumbo, yaani akimaanisha ni lazima kwani alikotoka ni mbali ukiachana na vikwazo alivyopitia. leo kwa kauli ileile msaidizi wake anasema Kaitaba ni lazima. kauli hiyo inachagizwa na maandalizi ya timu hiyo kwani kila mchezaji ana morali ya kushinda mchezo, 
       Unawaona vijana wa Masimango, hao ni baadhi wakiwa kwenye mazoezi yao ya mwisho kabla ya kwenda kuchukua point 3 muhimu.tathimini inaonesha kuwa KSC ina 90% kushinda mchezo huo ikiwa kikosi kitakamilika. hao unaowaona hapo ni viungo matata na ni kombinesheni hatari sana itakayojazwa na fidolin na Amos 'baloteli' hapo kati ni mwendo wa kukaba na kutoa pasi tu. ikiwa tathmini nii itakuwa sawa basi amini KSC ndio mabingwa wa wilaya Muleba 2016. Nawaalika wapenzi na wadau wote wa KSC muambatane na timu kishangilia zaidi. usikose habari za michezo kila siku kuhusu KSC kwa kutembelea mkamilo89.blogspot.com

Ijumaa, 7 Oktoba 2016

Kwa ukuta huu Victor apae angani

 kiungo ningeweka Amos (Baloteli) kayana,lameki na Fidolini, huku mastraika wangu wangekuwa Mashoto J na kapirima, 
     kaa hapo hapo kupata sportnews from Kamachumu
 usiache kutoa maoni yako kwa kutembelea Mkamilo89.blogspot.com

Kikosi kilichoipeleka KSC nusu fainal chini ya kocha mkuu Phyneous M. na msaidizi Jackson M, ligi ya wilaya 2016


Mlinda mlango ni Jawadu,walinzi ni Kaijage 'the stopper',Flolian,David na Ramso. huku viungo ni Amos'baloteli' Gilbert'middle'kayana na Fidolin huku washamuliaji ni Kapirima na Mashoto J.
         Kabla ya mchezo huo kuanza kutimua vumbi katika uwanja wa Zimbihile mjini muleba, kati ya Kamachumu sport club(KSC) na timu ya Muleba herroes,. alisikika nahodha wa timu Gilbert Jovino(aliyesimama wa kwanza kulia) akimwambia kocha wake "baba leo kufa na kupona". kama ambavyo manahodha wa timu mbalimbali kuhakikisha wanatimiza majukumu yao , alionekana kuwahamasisha wachezaji wenzake kuhakikisha kuwa wanamaliza mchezo mapema sana, alisikika pia kocha mkuu akisema "Mimi nataka goli 2 tu nyingine za heshima tu," unajua Masimango si mtu wa maneno mengi.       
       waliingia uwanjani na mwamuzi wa kati kuanzisha mapambano huku muleba Herroes wakionekana kama wanahitaji point 3 japo safari yao ilikuwa imekwisha. Walitaka kuharibu pilau la KSC, dakika ya 17 hali isiyo ya kawaida kwa straika J mashoto alikosa goli la wazi na hii inatafsiriwa na kocha kuwa presha ya mchezo kwani alipania sana kufunga, hali hiyo haikumtoa mchezoni straika huyu kwani alionekana kuwa mwiba kwa mabeki wa Herroes, dakika ya 35 nahodha Jovino 'middle' aliiandikia KSC goli la kwanza akiunganisha kross nzuri kutoka kwa Mashoto, cha ajabu mashabiki hawakushangilia goli hilo kwani kiu yao ilkuwa ni kumaliza kazi ya kupata goli 2 kipindi cha kwanza. hadi mapumziko KSC ilikuwa ikiongoza kwa goli moja, kocha alitumia dakika chache kurekebisha kikosi palipo na mapungufu, huku daktari wa timu Mkamilo G akiwatibu baadhi ya waliopata majeraha, morali ya mchezo ilikuwa kubwa sana kwa timu zote mbili kuwekeana tambo za hapa na pale.
         Naye meneja wa timu Malechela hakusita kutoa yake ya moyoni "jamani nina presha kubwa hapa na ninyi ndio wa kunitoa presha hii", twendeni tukamalizie kazi" ukitaka kuamini meneja huyu alidhamilia kuchukua ubingwa ni pale alipowaambia wachezaji muda wa kula katika moja ha hoteli hapo kamachumu mjini kuwa" vijana kuleni tu tutajua mbele kwa mbele" vijana walikula walivyoweza 
         kipindi cha pili kilianza kwa kasi sana huku nao Herroes wakionekana kama kuhitaji kupata goli la kusawazisha, hapo kati nakwambia si mchezo kwani ulipigwa mpira mwingi sana huku kiungo msumbufu ananyumbulika kila kona maarufu kwa jina 'baloteli' akiwapa shida wapinzani alikaba na kutoa pasi matata sana dakika ya 56 kanzaga kayana alipiga shuti kali na kumbabatiza mlinda mlango wa Herroes huku mashabiki wa KSC wakiamini kuwa biashara ilikuwa inakwisha, kazi ndio kama ilikuwa inaanza.
        dakiaka ya 64 Yuleyule aliyemkosa kipa dakika ya 17 straika Mashoto hakufanya ajizi mara baada ya kupata pasi nzuri kutoka 'middle' na kuuzamisha moja kwa moja wavuni sasa hapo ndipo benchi la ufundi la KSC na mashabiki wake waliinuka na kushangilia huku safu ya ulinzi ikionozwa na kaijage wakiwekeana malengo makali sana kuminda kipa ili wasipate madhara,
       dakika ya 73  kocha alifanya badiliko la pili kumpatia nafasi kiungo mkabaji kijana Daudi ili kuongeza nguvu ya kiungo mashabiki walishangilia sana kuona Daudi anaingia uwanjani kwani waliamini kazi yake si ya mchezo, ni kijana mfupi lakini usipokuwa makini utaumbuka uwanjani. dakika ya 80 kijana daudi manusura afanye kile alichokifanya Tambwe wikiend iliyopita kitu kilichowaacha hoi mashabiki, mbali ya kuwa ni mfupi na mwenye umbo dogo lakini walikiona hapo katikati, alikaba kama Mbuyu twite. 
       unajua kocha Masimango wakati mwingine ni kama aliamua kuweka historia katika ligi kwa kile alichokifanya, unajua nini? dakika moja ya nyongeza anafanya mabadiliko na kumpatia nafasi Hambali aliye onekana akipasha kwa hamu kubwa, ile anaingia hata hajafika katikati ya dimba la Zimbihile mwamuzi a mchezo huo alionekana akipuliza pye! pye!! pye!!!. hapo ndipo alisikika kocha mkuu akisema "Ooyoo!!!!!!!" nahodha "Ooyoo" vijana walitoka walipongezana ndani ya uwanja na kumshukuru MUNGU kuwajalia kumaliza mchezo salama na kuwafikisha nusu fainali. 
      alisikika pia kocha Masimango akisema "The issue is over, let's think about 'Kaitaba' meneja alifurahi kama ilivyokuwa siku ya mechi ya pili timu ilipocheza na vatikcan alipovaa jezi ya juu kichwani. majira ya saa 12:35 jioni wanapanda gari na kurudi mjini kwao kwani si unajua watoto wa mjini awalali njaa. 
            sasa nani ni nani mchezo wa nusu fainali kaa hapahapa nami Mkamilo89.blogspot.com 

Alhamisi, 6 Oktoba 2016

Beki wa kati wa Kamachumu sc (KSC) Moses Kuyela aimalika baada ya kupewa wiki 2 kutibiwa tatizo lake la enka

Habari za ndani za timu hiyo kupitia kwa msemaji wa KSC zinadai kuwa daktari wa timu Mkamilo GH amethibitisha kuimalika kwa beki huyo tegemezi wa timu hiyo hasa kwa hatua ilipofikia daktari asikika akisema " Afya ya beki kuyela ipo sawa na anafanya mazoezi mepesi kwa ajili ya kuingia nusu fainali itakayochezwa tar.08 au 09 0ctober2016,  alikosa michezo miwili ya liagi kutokana na majeraha aliyoyapat asiku ya mechi yao na Veteram V"
       sasa itakuwaje kama wakikutana na  Vietnam V? hapo mpira mwingisana utapigwa,
                   usiku wa deni haukawii kwisha

Ukitaka kuwa MKRISTO kubali na kuwa mtumwa!!

Kama YESU mwenyewe alivyokubali kuwa mtumwa kadhalika nasi pia imetupasa kuwa watumwail
i  yeyeatungezee njia nzuri ya kufika mbinguni, ni utumwa kiasi gani aliuonesha YESU kwetu, kudhalilishwa mbele ya watu wa jinsi zote na  rika zote, ni maumivu kiasi gani aliyapata kwa kupigiliwa misumari msalabani na kuchomwa ubavuni? unadhani siki kali huweza kufifisha kiu ya maji? ni wangapi leo wakila pilipili cha kwanza hukimbilia maji wanywe ili kupooza kiu? lakini fikiri jinsi iilivyo kiu ya maji nawe unapewa siki kali, je huu si zaidi ya utumwa? hakuwa na dhambi lakini aliitwa mdhambi, ni wangapi leo hii mtu akiba hukataa hata kuapa kwa mbingu, huyo ameiba lakini hukataa, YESU alikubali kuitwa mdhambi ni kwa kuwa aitamani kuwa mtumwa kwani alihakiki kuwa yeye kuwa mtumwa atatimiza ahadi aliyoahidi kwa baba yake kuwa "nitume mimi naminitakwenda kuyafanya yaliyo mapenzi yako" ni kweli alikuwa na nguvu ya ki-MUNGU lakin alikuwa na mwili wanyama kama mimi na wewe, alikula chakula kama mimi, alitembea na kulala kama mimi pia.
Ni ambo gumu kiasi gani kwa mwanaume kuwa wazi tena mbele jinsi na rika tofauti? hayo yote aliyavumilia kwa kuwa alitaka kumkomboa  mdhambi(mimi na wewe)
ni mara ngapi tunakosa na kusahau maumivu aliyyapata YESU? au tunafikiri ni maadhishi tu!!!
kuwa mKRISTO si sababu ya kuuona ufalme wa MUNGU, maisha ya kiKRISTO ndiyo ishara pekee ya kutupeleka mbinguni.
          tuwapende na kuwahudumia wengine, kuwajali,kuwathamini, kuwaona kuwa wao ni kaka mimi, kuwachukulia mizigo yao, kuwaombea rehema na maisha marefu. kuwaombea msamaha kwa wakosaji. kuwaombea mafanikio zaidi. lililio kuu katika yote hayo ni upendo, nao udumu kati yetu siku zote, huku tukiyatoa maisha yetu kuwa watumwa kwa ajili ya wengine,
                                          MUNGU na awe nanyi daima

Jumanne, 4 Oktoba 2016

"Tulikotoka ni mbali"

"hapa tulipo ni njiani ambako hata mwisho wa safari sijui, wewe wajua?" kila sekunde ya mbele isiyojulikana mdundo wake huwa kama ambavyo mapigo ya moyo wangu, lakini naketi pembezoni mwa njia panda na kujiuliza kwa nini waliogundua saa wameweka sekunde hizo mithili ya mapigo ya moyo wa mnyama. kwa ninini!!!  kuna wakati mkimbizi hukimbia hata asijue wapi anaelekea lengo lake ni kuwa huru. jamani tulikotoka ni mbali sana. 
kwani safari yetu ilianzia tumboni? au ni tulipozaliwa ,la hasha huko si mwanzo wa safari yetu, safari yetu ni ndefu sana na huenda hakuna ajuaye mwanzo huu. ni wazi wengi tunajua mwanzo wa mnyama ni utuogo wa mimba, lakini si wanzo wake, ndio maana hata hatujui siku ya mwisho wetu na ni wapi makazi yetu tukimaliza safari hii. sisi sote tuko safarini hata kama umejenga angani au baharini lakini upo safarini. kuna mmoja mkirbu na myahudi na mwingine myunani hawa wote sio wasafiri ? na yule mperizi si huyo msafiri? sasa kwanini kupanda muembe hali ikiwa unahitaji kula machungwa laini? tena iwaje kulima karangaikiwa hitaji lako ni ufuta? kilicho ndani yako ndicho kinukacho au kinukiacho? majeshi hupigana wakati wa vita kama ambavyo mtu hula akihisi njaa na kamwe hakuna alaye kwa niaba ya mwingine,ni mjamzito tu.Sasa tukijua hayo si vyema kujidharau na kumdharau mwingine, mpende na kumheshimu kila mtu na hasa kumsaidia kila uwezaye.