Jumapili, 20 Novemba 2016

Masimango,Mayanja: Std United unapeleka salamu lakini tusibweteke


Ni jambo ambalo halikutegemewa na wengi katikati ya jiji dogo laKamachumu kuwa timu yao ya KSC ingeweza kuchomoka mbele ya mechi iliyoisha muda mfupi hivi akribuni lakini kwa Imani ya makocha wao Mr Masimango na Mayanja waliamini tu kuwa kila kitu kitaenda sawa mabli na wapinzani wao kuwabeza.
     Ni dhahiri kuwa Masimango huamini mara zote katika kushinda kuliko kushindwa na hii ni Falsafa ya makocha wengi hasa wahispaniola na waholand ukiachana wale wa kijerumani ambao hata sekunde ya mwisho wao huona ndio fursa zao kumaliza kazi. sasa hii ni hali ya Kocha Mayanja anayeamini ukubwa wa pua si wingi wa......
Ni mechi iliyoisha kwa sare ya bila kutikisa wavu hata mara moja kati ya timu wenyeji KSC  na timu B ya Std United chama la wana  kutoka Shinyanga, haikuwa kazi rahisi kwa vijana wa Masimango kumaliza kazi hiyo kwani wengi wao hawakufika katika mchezo huo kutokana na matatizo ya kifamilia na kuugua ghafla, lakini waliokuwepo waliuhakikishia umati mkubwa uliofika kutazama mechi hiyo kuwa "Msituchukulie poapoa" na kweli wasichukuliwe poapoa.
chama la wana kama walidhani ni kazi ya kitoto kuwafunga vujana wa Mayanja basi watawapelekea ujumbe nao Azam Fc ili waje wakutane na kikosi kilichokamilika waone mziki wa Masimango.  kila aliyekuja uwanjani aliburudika na mchezo huo kwani ulikuwa wa kuvutia sana ukizingatia vijana wanajipanga kucheza ligi ya mkoa mapema mwezi ujao,inaleta matumani.
Kocha masimango mara baada ya mchezo kuisha aliwapongeza vijana wake na kuwaambia kuwa " Huu ni mwanzo tu wa kazi yenu nami nasema hiki si kiwango ambacho ninakihitaji, hatujafikia, hivyo msibweteke kudroo na Std United" hakuwa na maneno mengi
Naye kocha Mayanja aliwapongeza na kuwaambia " Vijana wangu jambo mlilolifanya leo sijalipenda hata kama hatukufungwa, jitahidini kuwa na nidhamu katika soka, nidhamu yenu iko chini sana na haiendezi. haiwezekani wageni wanatoka mbali na kuja hapa sisi hata mmoja hayupo, jambo hili limenikera sana na sitapenda lijirudie tena" alimalizia kwa kusema kuwa "jumapili ijayo tuna mechi nyingine kati yetu na simba B au Azam B, sasa kuanzia jnne hadi Ijumaa ni mazoezi makali na asiyekuja amejitoa, nawatakia jumapili njema na mapumziko mema"

                                                                                 Usikose kutembelea blog yako                                                                                                                      mkamilo89@blogspot.com

Jumapili, 13 Novemba 2016

Mkamilo:Tafrija hii lazima iwe ishara ya kucheza fainali ligi ya mkoa- Kagera

Ni mara baada tu ya ligi kuisha kocha wa timu aliwapa muda wa wiki 2 vijana wake ili kupumzika, lakini sasa amerejea  kutoka mapumzikoni na kufanya jambo moja
         Huenda kuna jambo hulijui na mimi nataka nikueleze ulifahamu, mbali na makocha hawa kufanya kazi ya kufundisha mpira lakini wana taaluma zao mbalimbali, kocha mkuu(Masimango) ni kocha kitaaluma lakini ana taaluma nyingine ikiwemo "urbun Development,social and Welfare", taaluma ya ukufunzi wa mpira aliyoisomea Denmark na taaluma nyingine moja, na zote hizo ni ngazi ya Stashahada, sasa usishangae ukimkuta kanisani anapanga nota kwenye kinanda ukadhani ameingia mlango wa "ke" huko pia yumo vizuri. Msaidizi wake(Mayanja) ni kocha kitaaluma stage III(Astashahada) na  mwalimu masomo ya sayansi sekondari ngazi shahada ya kwanza, sasa unaona makocha wa KSC walivyoenda kitabu?
         Sasa nije katika mada. ikiwa leo ni siku yetu ya kufurahia hatua tuliyofikia katika mashindano ya ligi ya wilaya Muleba tuna kila sababu za kusema hiki ni kielelezo cha kucheza fainali ligi ya mkoa mwaka 2016 Dactari wa timu Mr, Mkamilo alibainisha kwamba "lengo la hafla hii isiwe kutumbuiza na kufurahi bila ya kuweka malengo chanya, ila hafla hii iwe ishara ya kucheza ligi ya mkoa" aliendelea kusema   "Ni kweli ligi ya wilaya tulijitahidi sana kwa kujitoa, na tuwashukuru zaidi makocha wetu waliojitoa muda wao na nguvu zao kutufikisha hapa tulipo kwani  haikuwa kazi rahisi, pamoja na hayo wafadhiri na kila mmoja aliyeshiriki kutuwezesha kufanikisha adhima hii shukrani zetu ziwafikie waliko, kilichobaki ni kujipanga kwa ajili ya kucheza fainali mkoani"
            Alimalizia kwa kusema " Naamini kila jambo linawezekana tukimtanguliza MUNGU wetu"

Jumatatu, 7 Novemba 2016

Herman:"Kifo Changu 01"

msimu huu ni mzuri sana hasa kwa waliowahi kuweka mbegu zao ardhini kwani ndio hasa wakati mzuri wa mvua hizi kustawisha mazao, hii hutokana na ukweli kwamba mvua za mwanzo ndizo za kupandia uchelewapo nazo huisha ama kupungua na kusababisha kutokumea vizuri kwa mazao yasipomwagiliwa kwa wakati maalumu.
         wakati huu ni mzuri pia kw akuweka malengo ya nini ufanye  wakati  wa kuvuna kwani pasipo kufanya hivyo utafika wakati wa kuvuna wala hujaandaa mahali ppa kuhifadhia mavubo yako na hii ni hatari sana kwani wengi wamepata hasara zaidi kwa kukosa kuandaa mahali pa kuhifadhi mavuno,kama ulivyoandaa shamba na mbegu kabla ya kupanda na hivyo wakati wa kuvuna, maandalizi ya wapi utayahifadhi mavuno ni muhimu.
          Nilipokuwa mdogo sana nilikuwa natamani sana kupanda gari na kupata raha wananayopata wanaosafiri kwenye gari, ilikuwa siku moja baba alipata likizo kwenda kuwasalimu bibi na ndugu zetu huko kijijini, nilisikia akisema na mama "safari hii nitakwenda na--------" sikuamini kama alinitaja kuwa nami nitapanda gari, si unajua maisha ya kijijini, gari unalisikia wakija wageni tena kwa mwaka mara 2. mapigo ya moyo yalibadilika ghafla huku furaha ikizidi, maongezi yao yalizidi huko chumbani nami nilikosa usingizi kwa kuwasikiliza huku kaka na dada zangu wakiwa fofofo, baba alipolala mimi sikulala usingizi mzuri kwani kila nilipoamka nakumbuka kuwa nitapanda gari wiki hii, kibaya zaidi ilikuwa ni jumatatu na jumamosi ndio baba alikuwa anasafiri, kwa kuwa mama alinambia nitaondoka na baba nilipaa wakati mgumu sana kusubiria hadi jumamosi, kila mara nilikuwa nafikiri juu ya hilo ilipofika ijumaa nilisikia------------
           Ni kweli tunawaandaa wanawake zetu kwa ajli ya kuongeza familia?( kuzaa) au hutokea ajali kazini? ukweli ni kwamba  maisha ya leo ya wanetu yanahusiana na maisha ya sisi wazazi tulipompata !!! mtoto akija kwa dharura ataishi katika mazingira ya dharura kadhalika. tumejiandaa kuwalea watoto ipasavyo?? tumeijianaaje kupokea matokeo yoyote katika mahusiano yetu? kuna totauti zipi kati ya mwanamke, msichana na binti? mwanaume na mvulana? mimi sikumbuki ni lini ilikuwa siku yangu ya kuzaliwa japo mama alinambia ni tarehe--------- ila mimi sijui siku hiyo, kwani hata siku ya kwanza kuanza kutamka japo kwa kutoeleweka nilianza kwa neno "ba  ba ba" sasa sijui baba ndo aliniweka miezi 9 tumboni!! na 75% watoto wote tunapoanza kutamka tunaanza na neno ba ba ba, kimsingi malezi ya mtoto huanza tangu siku ya kwanza ya yeye kutungwa, hapo malezi yake yanatakiwa kuanza kwa pande zote yaani baba na mama, kwani bila kufanya hivyo kuna jambo huweza likapungua kwa mtoto huyo? ni lipi kubwa zaidi kuzaa au kuolewa?kuoa??
         "Kifo Changu"  huu unaweza ukawa ukweli kwamba kuishi si lazima sana ila kula ni muhimu kwani mtu haishi  bila kula, ama ni faida sana kuwa na uhai kuliko kuishi tu maana kuna tofauti kubwa sana kati ya kuishi na uhai, kuna faida ipi kuvuta na kutoa pumzi(kupumua) kama huna uhai? kuihi kusilete uhakika wa uhai kwani japo tu vinategemeana.hiki ni kifo changu japo hakionekani. ni jambo la kufikirika sana unaposikia amepatwa na umauti yaani amefariki, na hapo ndipo kifo changu kilipo, kwa jinsi hali hii ilivyo sasa ni matumaini tu ya kuwa hai kwa miaka mingi japo kuishi kila mtu ataishi miaka mingi. sasa kuna faida zipi kuishi bila uhai?? nilivyo sasa tofauti na jana kadhalika na kesho, maisha yangu ya jana leo na hata kesho ni tofauti sana, kwani kila siku inajitegemea, nikiyakukbuka yale ya nyuma yananipa nguvu kuamini  kuwa hiki ndicho kifo changu  na kwa hali hii ni vizuri nikapunguza kula kwani uhai wangu hautegemei zaidi kula, kwa masikitiko makubwa sana nawaza juu ya kifo hiki japo sijui ni lini lakini sasa huu wakati wangu kwani nilichokiona hapo haahahaha ni kinanipa ishara ya kifo changu na kweli kinaniuliza na jibu sina ilaa................... karibu tena kwetu  mkamilo89@blogspot.com

Jumanne, 1 Novemba 2016

Mkamilo: serikali isiwasahau ma Afisa kilimo kiasi hiki

 Kilimo ni uti wa mgongo wa nchi yetu Tanzania na asilimia kubwa ya sisi watanzania tunategemea kilimo. kilimo hiki si cha kulima tu kama zamani ambapo hali ya ardhi yetu ilikuwa nzuri na yenye rutuba ya kutosha,kama kawaida katika kila jambo Elimu ni kitu muhimu sana na kwa kulitambua hilo serikali imesomesha wataalamu wa kilimo ili kuwapeleka katika maeneo mbalimbali kuisambaza elimu hiyo kwa wakulima na wanajamii wengine katika kuwezesha kilimo cha kisasa na chenye tija kwa jamii. 
ikumbukwe kuwa kilimo hiki ndicho kinachompa mwanajamii kula na kuuza kupata fedha ya kununua mahitaji mengine muhimu wa ajili ya kuishi. 
katika kuhakikisha kilimo cha Tanzania kinakuwa chenye tija serikali inaendelea kuajili wataalamu wa kilimo na ma Afisa kilimo kwa ajili ya kuendelea kuelimisha wakulima mbinu mbadala za kuinua kilimo hiki ili kila mkulima afurahie maisha ya kuwa mkulima katika nchi ya Tanzania.katika hili serikali naipongeza kujitahidi angalau kufikia kuajili wataalamu hawa hadi ngazi ya kijiji.ni kweli kuna uhitaji mkubwa sana wa elimu hii ya kilimo bora kusambazwa kwa wakulima.
Ombi kwa Serikali   "tusiwasahau ma Afisa kilimo kiasi hiki" jamani hakuna kazi iliyo na urahisi kila kazi ni ngumu urahisi unakuja tu pale uanapoipenda na kuridhika na kazi hiyo toka moyoni. nianze kuwapa pole ma bwana shamba na kuwashauri kuipenda kazi yenu na kuifanya kwa moyo wote kwan kazi yenu inataka zaidi kujitoa kuifanikisha , naiomba serikali yetu ya Tanzania iwakumbuke watumishi hawa kwani huku niwaonavyo wanaishi katika mazingira magumu sana, inafika mahali najiuliza ni kweli walipenda kazi hii au ni kwa kuwa hali ya maisha ni ngumu na wakaama kusomea fani hii? watumishi hawa ni marafiki zangu sana katika eneo ninaloishi na ukweli ni kwamba huwezi amini kama ni watumishi wa serikali, unamkuta afisa kilimo anatembea kutoka alikopanga chumba hadi kuwafikia wateja wake ambao ni wakulima ni mbali sana na ukweli kila utakaposema unapanga bado huwezi kuwa karibu na wakulima wote kwa mfano mtu anapangiwa kazi mtaa wa mwenge mjini dar es salaam lakini hapo hakuna nyumba ya ma watumishi wa idara yao na wala ya kupanga hakuna inampasa mtumishi huyu atafute popote pale ili aweze kuishi na kufanya kazi. Anapanga maeneo ya ubungo, sasa niambie mtumishi huyu kila siku anatakiwa awahudumie wakulima wake anatoka saa ngapi ubungo na kufika mwenge saa ngapi, kumbuka amepangwa kijijini maana huko ndiko kwenye wakulima na kilimo kinafanyika kwa asilimia kubwa hata kama mkulima anakaa mjini lakini  kilimo chake ni kijijini, kwa wasiofahamu mazingira niliyotolea mfano, ona na huu nao, mtumishi huyu amepangwa kazi kituo A lakini hakuna nyumba ya watumishi hata moja anaamua kutafuta huko kijiji jirani, anapata nyumba ya kuishi kilometa 4-8 kituo B kutoka katika kituo A hadi B anatumia muda gani?serikali msiwasahau kiasi hiki, wengi wao wanaishi maeneo ya mbali na vituo vyao kwani nyumba za kupanga hakuna, 
ma bwana shamba wa zamani nilikuwa nawaona wana pikipiki za kwenda kazini lakini kwa sasa hakuna ukiwaona ni wawiili katika 50, wanaishi mazingira magumu sana na mshahara ulivyo kidogo, ikifika tarehe 10 umekwisha hali hii si nzuri, huwa nawaona wamevaa mabuti kama wanakwenda kupigana kumbe ndio kazini kwao hadi huwa nacheka kwa huruma, akirudi jamaa kachoka hatari kwani mwendo aliotembea kwenda na kurudi ni kilomita si chini ya 7 na kuwatembelea wakulima si chini ya 2km, jamani bora ya sisi walimu tunaamka na kutembea kidogo tunafika darasani kufundisha japo nasi tuna changamoto kidogo ila hawa ma bwana kilimo ni zaidi, huwa namwona jamaa yangu wa kilimo ikinyesha mvua anarudi kalowa kama nini , mwalimu mvua ikinyesha anaendelea kufudisha ndani huyu anajihami kwenye majani ya migomba na wakulima wake ni ajabu sana. ma bwana shamba pazeni sauti ili nanyi msikike kama sisi walimu hatuchoki kuwakumbusha serikali kwani kunyamaza kimya hakuwezi kusaidia. japo kidogo wametusikia na wameanza kututimizia haki zetu tunaamini mh Magufuli utahakikisha tunaishi mazingira mazuri na hawa ma bwana kilimo msiwasahau kwani ni bora wangekuwa walimu tu huku alimu ni raha tu, nawasihi mvumilie na serikali iwanunulie pikipiki angalau na nyumba za kuishi katika kula kata kuepuka kukaa mbali na maeneo yenu ya kazi ni kweli tunahitaji huduma yaa kitaalam  zaidi ila mnapata shida kama sisi  weakati mwingine nilifikiri ni bora nimekuwa mwalimu kuliko kuwa bibi shamba nitakuwa mwalimu nitavumilia siku zote kwani kila kazi ina ugumu wake, nikiwaona madokta na manesi huwa narudi na kufikiri kama ningekuwa mimi kwa akili yangu ya hasira nisingekuwa sioshi madonda ya mwingine na kimshahara kadogo hivi? lakini wanajitoa siku zote kuhakikisha mgonjwa anapata huduma nzui na kupona kabisa, wakati mwingine hali za mahospitali ni mbaya sana, jamani kuokoa maisha ya mwingine inahitaji kujitoa pia, jamani walimu tulie lakini tukiangalia kwa wenzetu tutaona kuwa ni heri sisi kwani wanayoyapitia ni magumu pia, ni afadhali kabisa kwa watendaji na mahakimu sijui mawakili. nawaombeni serikalimkija kurekebisha mishahara tazameni ugumu wa kila kazi kuliko kuweka kiwango kimoja kwa kila ngazi, hawa wa kilimo wanateseka sana jamani kuzunguka kutwa yote na jua kali, nitabeba lundo la madaftari na kulisahihisha hat kwa masaa 5 sio kupigwa vumbi n jua, kilimo ni uti wa mgongo wa Tanzania
 poleni sana