Jumamosi, 8 Aprili 2017

Mpira huu!!!!!!!!!!!

Japo ni ukweli kamba hakuna aliye mkamilifu lakini madhaifu mengine ni kuyatafuta sisi wenyewe,
hapa ndipo tunapotaka tufikie kwa mpira wetu, naamini kuwa kuna kila sababu ya kupata watu wenye taaluma na mpira ili wasimamie mpira wetu tena sio wenye njaa, unajua mtu mwenye njaa hata akipewa ukoko wa wali ataona amepewa pilau, hiyo yote ni kwa kuwa alikuwa hajui ni wapi atapata chakula,
Sina maana watu wenye pesa ndio wasimamie mpira japo kwa angalau 40% iwe hivyo.
Jamani kila siku wadau wa mpira wetu wa Tz tunalalamikia vyombo vinavyosimamia huu mpira wetu kwa nini hamsikii? hamshauriki? hamkosoleki? naamini ili uwe kiongozi bora mahali popote ni lazima ukubali kushauriwa, kukosolewa na hata kunyoonyewa vidole vya unaowangoza na ikiwezekana kwa weledi ww ukaomba ushauri kwa unaoamini wanaweza kukusadia,
Kila siku wadau tunatamani mpira wetu ufike mbali lakini kwa nn hatufiki mbali ni kwa sababu hatukubali kukosolewa kuwa hapa tumekosea na tutazame namna ya kusahihisha.tunatamani siku moja tupaze sauti zetu tuseme Malinzi baba tunakshukuru kwa kazi nzuri lkn sio kila siku watu wanatamani muda wako uishe wamchague mwingine hali hii si nzuri hata kidogo. TFF ndiyo chombo kikubwa cha kusimamia mpira wetu na ndio maana kila mzigo wa lawama.
          Hivi bodi ya ligi katika jambo hili hata tukiwabatiza majina yasiyo yenu msitulaumu, kwa nn mnapenda kuingiza siasa kwenye mpira, unajua mpira ni sayansi makini, inataka hesabu za ukweli tena za muda husika. mpira sio sio kazi ndogo ni kazi ya umakini sana,
       Tukiacha matukio yaliyopita tuone hili la juzi la mechi ya simba na kagera kule kaitaba bukoba,. kuna malalamiko ya kucheza kwa beki wa Kagera aitwaye Fakhi wakati inaelezwa kuwa anatumikia kadi tatu za njano, lalamiko hilo limeshafika bodi ya ligi siku tatu  sasa na leo mnasema litatolewa ufafanuzi siku ya alhamisi, hivi mnaposema kuwa ufafanuzi ni siku ya alhamisi mna sababu gani ya msingi? nafikiri suala si kuangalia mechi gani alionywa kadi hizo inayomzuia asicheze mechi inayofuata siyo? si ni suala la kupitia kumbukumbu za mechi tu jamani?? au kuna hitaji la kupeana semina elekezi hapo? Au mnataka Kagera waje muanze mvutano?? masaa 72 hayakutosha kumaliza jambo hilo??
 lakini bodi la ligi hamkumbuki kuwa mna jukumu la kuhakikisha mnapitia majina ya wachezaji waliopewa kadi na kutoa taarifa kuwa wachezaji fulani hawataruhusiwa  kucheza mechi fulani mkiainisha sababu?? ni kama walivyofanya CAF kwa yanga mechi ya marudiano dhidi ya Ngaya FC, Yanga walipewa taarifa kuomumia Donald Ngoma kwa kuwa alikuwa na kadi 3 za njano. sasa vipi huku kwetu?? japo pia ni suala la kocha wa tim na meneja na ikiwezekana hata nahodha wa timu anapaswa kusimamia jambo hili lakini mwisho wa yote Bodi ya ligi mnapaswa kuzingatia hilo maana ninyi ndio wasimamiz wa mwisho wa mambo haya.
ni kama mechi ya Yanga VS Azam, ilikuwa ni mechi muhimu sana kwao kupata point 3, lakini  waligundua kuwa wachezaji wao muhimu  Hassan kessy na Kelvin Yondani walikuwa na kadi 3 za njano na Yanga hawakuona sababu ya kuwatumia, ni jambo dogo sana kutunza kumbukumbu hizi ili kutoweka mashaka ya point za mezani jamani.
Je kama Simba wasingelalamika sheria haichukui mkondo wake, au sheria iko kazini hadi pawe na malalamiko. kwa kweli bodi ya ligi na TFF mnayumbisha mpira hebu tazameni ratiba zenu zilivyo. kila siku madudu yanatokea huko, sasa jambo limefika kwenu ni kazi ngumu kupitia hizo kukbukumbu na kutoa majibu??? maana maxime na meneja wa imu ya Kagera wanaamini na uhakika kuwa mchezaji wao ana kadi 2 tu na Uonguz wa simba uansema kuwa Fakhi alikuwa na kadi 3 ili kupata jibu wanakuja kwenu sasa kazi ya masaa mawili mnaifanya kwa wiki 2 jamani tutafika na hii kasi ya ..........!!!!!!
           Nanyi viongozi wa Simba hamkuwa mnajua kwamba Fakhi ana kadi 3 za njano?? maana mlipomaliza mchezo ndio mkaanza kutoa malalamiko, nanyi mnaonesha ni jinsi gani hamko makini kwa kazi yenu,  au mlikuwa hamna uhakika wa kushinda mechi hiyo sasa mkaona lolote linweze kutokea. mchezo mbaya huo.
rufaa ya mchezaji wa African Lyon hadi leo  iko kapuni au mnataka kuamua rufaa hizi ikiwa imebaki mechi moja kumaliza ligi?? maana yanga nao walikata rufaa juu ya mchezaji ambaye usajiri wake ulikuwa hujakamilika, lakini  miezi 2 sasa iko kapuni, lakini hali hii itaisha lini??

    Nawaomba wahusika malizeni hizi kazi mapema ili msitengeneze maswali mengi kwetu tunaofuatilia na kulinganisha.