Jumamosi, 27 Mei 2017

"Mkumbuke na kumtumikia MUNGU siku zote za ujana wako"

Mwanadamu ni mavumbi na mavumbini wote tutarudi' tukiwa katiak uhai huu kwa mapenzi ya MUNGU inatubidi kwa hali ya juu kuutafuta utakatifu ambao Bwana YESU ametupatia kupitia kifo chake. 
Amani na imani zaidi ni Upendo viwe tenzi zetu za rohoni wakati wote kwani katika hili utukufu wa MUNGU mwenyewe unang'aa kila mahali.
Mpende jirani yako kama nafsi yako, ukimpenda kwa moyo wako wote utamfanikishia hata yasiyouwezo wake. 
Nami namkumbusha Marchela Mwamunyi(Master) ajiandae bila kuwa na sababu yoyote ama kikwazo aende kanisani kesho akasali pamoja na waaamini wenzake na sio kusali peke yake uwanjani, huu ni wito kwangu kwako marchela kwani nakupenda sana na ili nisimamie ndoa yako mwakani ni lazima uanze kwenda kanisani.
Kwa nini nisikwambie ukweli kama nakupenda? Na katika kumpatia ujumbe naye kwa kuamini kwake akanijulisha nisome "2kor:4:6-8, na 6:4:8" katika haya yote akiwa na ujumbe.........

"Kwa kuwa Mungu, aliyesema, Nuru itang'aa toka gizani, ndiye aliyeng'aa mioyoni mwetu, atupe nuru ya elimu ya utukufu wa Mungu katika uso wa Yesu Kristo
MUNGU humtoa aliye gizani na kumtakasa, kama alivyomtoa Daudi katika kundi la ng'ombe na kumfanya kuwa Mfalme.
mimi na wewe tupo gizani ungana na Marchela mwamunyi  tumrudie MUNGU siku za ujana wetu. 

Mkamilo

Jumanne, 23 Mei 2017

"MANJI FIKIRI UPYA" SI SAHIHI KWA SASA

 

Kuna wakati ambapo watu hufikiri kuwa hakuna MUNGU kutokana na ugumu wa maisha wanayopitia . hapo ni sekunde moja ya mapitio haya lakini kuna sauti ya mwingine husema maisha ni jaribio na kama utaweka thamani kwa kila hatua basi jaribio hilo litafanikiwa. 
Yuko mwandishi myudea  aliitwa Amarcus `Onsentumrcus aliwahi kusema "Ombertudas O~uternun osceyum" akiimaanisha "My Experiment value My Life" katika jarida lake la mwaka 1729 aliweka wazi dhamira yake ya kuyaweka maisha yake katika kila jaribio kwa miaka 30 huku akiamini anaweza kuishi miaka 98 akiwa na nguvu ya kuponda vyuma na ndipo kabla ya kufikia miaka hiyo alikutana na tajiri mmoja aliyempa kazi ya ukuu katika karakana moja kubwa nchini humo.kwa kuwa Ombertudas alikuwa katika kipindi cha Life Experiment hakukubali ombi la kazi hiyo kwa kuwa muda wake wa Experiment hakuhitaji. aliendelea na msimamo wake huku akiamini atrafikisha miaka 98 kwani ndio lilikuwa lengo lake katika jaribio, 
Ni makala kubwa sana kwake lakini kitu gani napenda tujifunze kwa huyu bwana,Ni kuyaishi maisha ya kweli katika uaminifu, Zaidi ni kutunza ahadi ambazo kila mtu anajiwekea. 
Mh.Manji nakusihi kwa kuwa uliweka ahadi ya kuisaidia Yanga hadi mwisho wa nguvu zako, sasa tunza ahadi yako kwa moyo wote nami naamini hili limetokanan na udhamini wa SPORTPESA. lakini  hili limekuja ili kutusaidia katika kuundesha mpira wetu, Ndugu Manji sisi kama wadau wako tumekuwa na huzuni kwa kipindi chote cha misukosuko yako nasi tukiamini kuwa siku moja yataisha tukafurahi pamoja, na vijana walipambana mwanzo mwisho hadi kupata Ubingwa  2016-2017 na hii ni zawadi kwako M/kiti wetu. Sasa leo umeamua kufanya hayo maamuzi nasi tunaamini kuwa umeumia sana kwa hilo. 
lakini nakuandikia kwamba FIKIRI UPYA

Bado Tunathamini sana huduma yako na bado tunathamini mchango wako mkubwa sana. 
ukiwa baba FIKIRI UPYA

G. mkamilo


Alhamisi, 11 Mei 2017

"TAZAMA RAMANI UTAONA NCHI NZURI"



                                     "Tazama ramani utaona nzchi nzuri, yenye mito milima mabonde yapendeza,                                  majira yrtu haya yamekuaje sasa utumwa wa Nchi Nyerere ameukomesha............"


Kila kilichopo mwanzo ni wazi sasa kina Simulizi yake na hata vile vijavyo kamwe havitakosa Simulizi. huu ndio usemi wa kuwa kila kitu kuwapo au kutokuwapo kwake kunategemeaSimulizi, watu wanaposimulia Simulizi hizi husahau kuwa kuna Hadithi tamu ambazo hufifisha mawazo kwa msemo ya sukari lakini ukweli utabaki kuwa mti mbichi ndio kuni nzuri na kamwe husemi uongo kwa kanisa moja. mahali hapa si pachafu kama waajemi walivyokiri japo ni ukweli usiopingika kuwa zile hadithi zao ni kama zilifanana na simulizi za  Konkuu. N hii lijamu ni tamu sana wakati wa masika na kwa kuwa hutengenezwa kwa ajili hiyo wamesahau kuweka sukari.
          MUNGU hakuumba watu hapo mwanzo bali alimuumba mwanadamu Adamu, sasa  watu wamezaliwa baada ya hapo,
Katika hili hakuna wa kulaumiwa kwani hata wazee wa kenda hawakujua kuwa huyu si mwanadamu bali ni MUNGU muumba wa kila kitu. hakuna apikaye mchele usonukia akachezesha pua yake. mlevi wa pombe je, unaweza mnunulia soda akakushukuru? SHUKRANII!!!
          MUNGU anasema nasi kuwa " shukuruni kwa kila jambo tena shukuruni"  Kwa wanaoamini kwa MUNGU huelewa ni jinsi gani MUNGU anahimiza KUSHUKURU, katika kushukuru ni wazi pasiwepo na neno lakini kwa kuwa kuwepo kwa neno hilo kunaondoa thamani ya shukrani yenyewe.
        Mlima huu ni mrefu sana kuupanda bila kuwa na ngazi na akiba ya maji ya kunywa kwani jasho huenda likavuja sana na kuhisi kupata hamu ya kunywa, lakini hii baridi huashiria kuna kitu.kushukuru ni jambo muhim sana na lenye maana kubwa.
haijarishi shida gani imekupata au matatizo gani yamekusibu lakini wito mkuu leo ni kushukuru kwa kila jambo.
Ni mabadiriko makubwa sana yanatokea kwa chma kuyeyuka na kuwa sahani, hupitia kwenye moto na kisha kulainika
Naamini katika mabadiliko, hata MUNGU aliweka mabadiliko mbalimbali, nasi lazima tuamini katik hayo,.
katika maendeleo yoyote yale ipo simulizi ya maendeleo yale lakini si hadithi la hasha. Mabadiliko ni lazima yaendane na maumivu, ukiona huna maumivu katika mabadiliko hayo basi hakuna tena mabadiliko hapo.Hebu ona asili ya mwanadamu kuwa ni udongo, je huu udongo ulibadili rangi ya kuwa mweusi au mzungu/mweupe? lakini katika hili hakuna wa kujibu.
Sasa Nelsoni Mandela alipotamani kuweka mabadiliko Nchini Afrika kusini ilimlazimu akubali kuingia  na kufungwa jela miaka mingi, hapo ni maumivu kiasi gani kwa mtu kuifia Nchi, je ni nani awezaye kuyafanya hayo kwa sasa, je hiyo ni Hadithi kweli?? huyu Muammali Gadaff aliamua kuifia nchi masikini ili siku moja iwe tajiri, Nchi isio na rutuba aliutoa udongo mbali na kuijenga nchi lakini ndo huyo aliyepigwa na kuuawa kama mwizi.
Hayo ni sehemu ya mabadiliko tu, na ukweli ni kwamba hakuna aliyekubali kushindwa kabla kufika safari aliyotarajia kufika.
Kwetu Tanzania ni miaka mingi tumekuwa tukilalamika kuwa tunataka mabadiliko. Tulipaza sauti za MABADILIKO!, MABADILIKO!! MABADILIKO!!! Na moja ya sera ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kila kona kulisikika neno MABADILIKO,. na baada ya uchaguzi kuisha hakukusikika neno mabadiliko tena. je ni kweli kuwa MABADILIKO yametimia?
Naamini kuwa bado hayajatimia ila yapo taratibu.
tangu Serikali ya awamu ya tano imeanza kazi kuana mabadiliko kadhaa ya mejitokeza, la kwanza ni lile la kusimamia kauli na kutekeleza yaani kusema kuwa nataka A na kweli A inafanyika. tunaona kasi kubwa ya utendaji maofisini,  hata kama wengine wanafanya kwa woga lakini ndio mabadiliko hayo.
Watu wanataka kazi tu.na Mh. anataka kazi tu!! sasa na hili la ukaguzi wa Vyeti feki ni kazi tu!!!
katika kuyapokea mabadiliko lazima kutakuwa na maumivu makubwa.Mh. kwa dhamira nzuri ameamua kuondoa kazini wale wote wenye vyeti feki na hapo ndipo maumivu ya moyo hujaa zaidi kwani ni ukweli usiopingika kuwa hakuna anayeyafurahia mabadiliko haya hata kama ni mwana CCM damu lakini ukweli utabaki palepale kuwa haya ni mabadiliko, unadhani Marehemu Nelsoni Mandelaa alifurahia kukaa jera miaka kenda tena kwa ajili ya wana Afrika Kusini??? gadaff alikubali kuuawa kinyama kwa sababu ya Libya yake. sasa mimi na wewe unadhani ni rahisi kucheka unapokosa kujua kesho yako iko wapi ikiwa ilikuwa unaamka na kuingia ofsini tena unakuta mahususi wako amekuwekea chai na mkate wa blueband sasa unaamka na kuangalia jogoo anawika bila sauti nzuri.
haya pia ni mabadiliko, ulizoea kupata pesa kila mwezi lakini sasa unapiga hesabu za kupata kila wiki lakini zilizo na masharti. "NINGEJUA MAPEMA,  NINGE........... " Hii ni kauli wengi huikumbuka sasa hivi. lakini sisi ndio tuliokuwa tunazungusha mikono yetu mwaka 2015 kusema MABADILIKOOOOOO Yaanziekwangu, na Mh sasa ameanzisha mabadiliko. Big Up Mh. kwa kusikia kilio cha watanzania na kuwatimizia haja ya mioyo yao. nachokupenda Mh. ni kuwa ww ni msikivu sana na kila mtu naamini anakupenda katika hilo la kuwa msikivu.
 kwaniumeamua kucheza ngoma 2 kwa wakati mmoja na sasa kil mtu anasema wewe ni shujaa.
          Jamani wazazi hata mimi naandika naumia sana kuona mwingine anakosa kazi lakini sasa nitafanyaje na wakati  hata mimi mwaka 2015 nilizungusha mikono kusema nataka mabadiliko, nitamlaumu nani ikiwa mimi ndiye niliyaomba haya.
Ipo hivi maandiko yanasema wazi (Mathayo 7:7) Ombeni nanyi Mtapewa, tafuteni Nanyi Mtaona, bisheni hodi Nanyi mtafunguliwa. kwa maana kila aombaye hupokea, sasa nami nasema kuwa tuliomba na sasa mh ametupatia. wengine husema oooh jamani kimi sikuomba mabadiliko, lakini kumbuka kuwa hata MUNGU anasema muwaombee wasioweza kuomba., kila mtu na ambuomee mwenzake na huo ndio upendo kwani hata wanaoamini kawa YESU KRISTO aliwaombea wote na kuwa okoa wanadamu wote.
wewe usiyeomba haya elewa kwamba yupo aliyeomba kwa niaba yako. Naamini mlioguswa na jambo hili pamoja na familia zenu mna huzuni kubwa sana lakini umbuka kuwa MUNGU kasema  SHUKURU  kwa kila jambo. Ni kweli kuwa jambo hili limewaathiri wengi sana kisaiklojia sio tu waliokutwa na vyeti  feki ila kil mmoja  kuna watu wanne nyuma yake. sasa wapi kimbilio lao?? lakini huepuki hili neno mabadiliko.
wwazazi wanalia machozi mengi sana juu ya vijana wao waliokutwa na jambo hili lakini haya ni MABADILIKO, hapa ndoa zitavurugika, waliotaka kufunga ndoa wataghairi na kuachana, watoto waliokuwa wakisoma shule nzuri za vipaji watarudi huku kwetu, kuna athari nyingi za jambo hili , lakini hutaondoa maana ya neno MABADILIKO.  yuko mzee ana watoto 6 wote wanasoma sekondari za bweni na za kulipia, alibakiza miaka 2 kustaafu kazi na sasa  hajajenga hata kibanda alikuwa akiishi kwenye nyumba za serikali na familia yake, hebu nambie tunategemea nini kwa mzee huyu? je maana ya neno MABADILIKO litakufa??? sasa huyu mama mjane mwingine aliyesomesha  watoto wake wawili kwa kuuza kalimati na ashikilimu kwa miaka 10 hakujenga wala kununua shamba akimwamini MUNGU kuwa ipo siku atafankiwa kupitia watoto hawa , walipata kazi mwaka 2015 na sasa wapo katika orodha ya vyeti feki, unatoa jibu gani kwa mama huyu ambaye nywele zake ziana mvi lukuki??? lakini kamwe neno MABADILIKO huwezi liweka kapuni kwa kuwa hata pilato aliwaambia mayahudi kuwa " Nililoandiak nimeandika"
Watu tunawaza mengi sana juu ya jambo hili lakini ukweli utabaki kuzungusha mikono na hata twe na maumivu kiasi gani ukweli huu haupiti bure. hatufanani katika kufikiri hivyo ni vyema kuheshimu mawazo ya kila mtu japo kuyakubali ni maamuzi binafsi.
 wapo wanaosema mbona mawaziri, wabunge, madiwani, wakuu wa mikoa na wilaya kawaacha? huenda hatujui jambo lakini yy ndie mkuu wa nchi na huenda kabla hajawateua aliwakagua kwanza na swali lipo kwa wabunge a madiwani ambao walipigiwa kura je sio watumishi, maana ya mtumishi ni mtu anayetumwa, je makundi hayo hayatumwi???  hata naswali haya hayaondoi maana ya neno MABADILIKO.
OMBI langu kwako Mh. mimi nikiwa mwalimu, furaha yangu kubwa ni kuona wanafunzi wangu wanaelewa vizuri na kufaulu mitihani mbalimbali, sasa nikiona wanafunzi hawaelewi ni lazima nijiulize kwa nini hawaelewi na kisha kuruda kufundisha somo hilo. Sasa nami naomba ikiwezekana waeleweshe wanafunzi wako vi
zuri waelewe kwa nin ukaguzi huu hauwahusu makundi hayo kama wabunge, ma RC, DC na mawaziri? ili wakielewa siku nyingine wasiulize.
Lakini pia nina ombi katika Ofisi yako, kuwa  kuna mwalimu mwenye cheti feki amabye alimfundisha mwanafunzi ambaye sasa ni daktari mahiri sana mwenye vyeti visafi kabisa, je hili likoje?? japo ni wazi kuwa siwezi ondoa maana ya neno MABADILIKO. si maandiko husema kila aombaye hupokea, ikikupendeza nami nipokee.
wenye vyeti feki hutibu wagonjwa na kupona kabisa, husafirisha abirir kwa ndege, hufundisha maprofesa na madokta, sasa hapa inakuwaje kwa kweli mimi ni mwanafunzi ambaye sujaelewa na kwa kuwa kuuliza si ujinga naomba kueleweshwa zaidi,.
 OMBI namba 2 ni kwamba, ikikupendeza Mh.wasamehe wote waliobakiza miaka 7 kustaafu kwani utakuwa umewasaidia sana, wamalize muda wao na wapate stahiki zao za kustaafu. nafikiri sisi tumejifunza kupitia jambo hili.  Nafahamu MABADILIKO hayazuiliki kwa kauli na ombi langu kwako.Lakini pia mimi nashkuru kwa kuwa una dhamira ya dhati ya kuitoa Tamzania hapa Ilipo.
Watanzania wenzangu tuombeane mema kwa kla jambo.
Nawatakia kazi njema za ujenzi wa taifa letu.
AAAMINAAA

Jumatatu, 8 Mei 2017

"MUNGU Awapumzishe kwa amani mahali Pema Peponi AAminaa!!!!"

" Mlale Pema Peponi Wapendwa Mlale Pemaa X 2 ( Taja majina yao)

1. Mlikuwa wapendwa wetu, wenye tumaini kubwa kwetu.
Muende salamaa
2. MUNGU wetu wa Huruma, awapokee Uwinguni Mpumzike salama.

Kwa kuwa wewe MUNGU  ndiye Muumba wa vyote nasi wanadamu tunajua kuwa hakuna kilichopo kisicho asili yako, uliyeweka ndiye utoaye, unayetengeneza na kuharibu,
Kwa masikitiko makubwa tumepokea msiba huu mzito wa taifa juu ya ndugu zetu wapendwa ambao wameitwa nawe MUNGU kupitia ajali ya gari, kuitwa huku kumetuacha na huzuni majonzi na simanzi kubwa mioyoni mwetu hasa tukifikiri muda wao mfupi walioishi hapa duniani.
wapendwa wetu wenye thamni kubwa sana hawakufahamu changamoto zozote na walikuwa kama malaika wasiojua kuna kufa hapa duniani, maisha yao siku zote yalikuwa ni ya furaha na hata walipokuwa kwenye safari yao hawakujua kuwa huo ni mwisho wa pumzi yao japo wewe MUNGU wetu kwa Imani sisi tunajua ulijua kuwa siku hiyo unawaita uwapumzishe kwenye raha ya milele.
Sisi kwa wanadamu tunapokea kwa masikitiko makubwa sana na machozi yetu wewe wayaona. kwa jambo hili pia tunakushukuru kwa kuwa umesema tushukuru kwa kila jambo hasa tukiamini kuwa Umewaita uwapumzishe. Tukiwa Watanzania tunazidi kukuomba utufariji na kutupa amani zaidi katika wakati huu mgumu wa maumivu. uwape amani wazazi na wanafunzi wenzao waliowaacha shuleni,
Hakika huu ni msiba wa Tanzania nzima, umetufikia wote nasi hatuna budi kuupokea kwani kazi yako Ewe MUNGU haina makosa.
Tuliwapenda,walitupenda lakini wewe MUNGU umewapenda zaidi.

          " ROHO ZA MAREHEMU WAPENDWA WETU ZIPATE REHEMA ZA MUNGU                              ZIPUMZIKE KWA AMANI< AAMINAA."

MKAMILO