Jumamosi, 27 Mei 2017

"Mkumbuke na kumtumikia MUNGU siku zote za ujana wako"

Mwanadamu ni mavumbi na mavumbini wote tutarudi' tukiwa katiak uhai huu kwa mapenzi ya MUNGU inatubidi kwa hali ya juu kuutafuta utakatifu ambao Bwana YESU ametupatia kupitia kifo chake. 
Amani na imani zaidi ni Upendo viwe tenzi zetu za rohoni wakati wote kwani katika hili utukufu wa MUNGU mwenyewe unang'aa kila mahali.
Mpende jirani yako kama nafsi yako, ukimpenda kwa moyo wako wote utamfanikishia hata yasiyouwezo wake. 
Nami namkumbusha Marchela Mwamunyi(Master) ajiandae bila kuwa na sababu yoyote ama kikwazo aende kanisani kesho akasali pamoja na waaamini wenzake na sio kusali peke yake uwanjani, huu ni wito kwangu kwako marchela kwani nakupenda sana na ili nisimamie ndoa yako mwakani ni lazima uanze kwenda kanisani.
Kwa nini nisikwambie ukweli kama nakupenda? Na katika kumpatia ujumbe naye kwa kuamini kwake akanijulisha nisome "2kor:4:6-8, na 6:4:8" katika haya yote akiwa na ujumbe.........

"Kwa kuwa Mungu, aliyesema, Nuru itang'aa toka gizani, ndiye aliyeng'aa mioyoni mwetu, atupe nuru ya elimu ya utukufu wa Mungu katika uso wa Yesu Kristo
MUNGU humtoa aliye gizani na kumtakasa, kama alivyomtoa Daudi katika kundi la ng'ombe na kumfanya kuwa Mfalme.
mimi na wewe tupo gizani ungana na Marchela mwamunyi  tumrudie MUNGU siku za ujana wetu. 

Mkamilo

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni